1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad: Maafa yaendelea nchini Iraq.

9 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtZ

Watu kumi na watatu wameuawa na wengine kumi na sita wamejeruhiwa baada ya shambulio la bomu lililolenga msikiti wa Kishia katika mji wa Kirkuk, kaskazini mwa Iraq.

Mabomu mawili yamelipuka kwa wakati mmoja na kuwaua watu kumi na sita na wengine thelathini na wawili wamejeruhiwa katika mji wa al-Khurna karibu na mji wa Basra, kusini mwa nchi hiyo.

Katika mkoa wa Diyala mashariki mwa Baghdad, watu waliokuwa na bunduki wamevamia nyumbani kwa afisa mmoja mkuu wa polisi wakamuua mkewe, ndugu yake na walinzi kumi na wawili na kisha wakawateka nyara watoto wake watatu.