1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mabomu yaripuka kaskazini mwa Irak

3 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVP

Nchini Irak,watu wasiopungua 2 wameuawa na wengine 40 wamejeruhiwa,baada ya mabomu manane ya gari kuripuka katika mji wa mafuta Kirkuk,ulio kaskazini mwa nchi.Mabomu 2 yalilenga ofisi za vyama viwili vikuu vya Wakurd.Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema,si jambo la kawaida kushuhudia mashambulio kaskazini mwa Irak na mashambulio haya sasa huenda yakazusha mivutano ya kikabila.Kwa upande mwingine,majeshi ya Kimarekani katika mji mkuu wa Irak,Baghdad wamesema,wamewaua wanamgambo 4 wa al-Qaeda.Wakati huo huo vikosi vya usalama vya Irak vimearifu kuwa vimegundua maiti 23 za watu wasiojulikana, ikiaminika kuwa watu hao ni wahanga wa mapigano, kati ya makundi ya jamii mbali mbali.Kwa upande mwingine,polisi mjini Samarra wamesema,waasi wamewaua makomando 4 wa polisi kwenye kituo cha ukaguzi katika barabara kuu.Kiongozi mkuu wa kidini wa madhehebu ya Kishia nchini Irak,Ali al-Sistani ametoa wito wa kuwa na umoja wa Kiislamu na kusitisha mgogoro wa kimadhehebu.