1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Maiti za wahanga wa mapigano ya kidini

8 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4x

Polisi katika mji mkuu wa Irak,Baghdad wamekuta maiti 51 katika kipindi cha siku moja.Baadhi kubwa ya watu hao waliteswa na kupigwa risasi.Maafisa wanadhani kuwa marehemu hao ni wahanga wa mapigano ya mjini Baghdad kati ya waasi wa Kisunni na wanamgambo wa Kishia.Takriban wanajeshi 50,000 wa Marekani na Irak waliotawanywa katika mji mkuu Baghdad peke yake,wameshindwa kuzuia mapambano yanyoendelea tangu miezi kadhaa kati ya makundi ya kidini.