1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Maiti zenye alama za mateso zimegunduliwa Irak

4 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwF

Polisi nchini Irak imesema hadi maiti 55 zimekutikana katika mji mkuu Baghdad katika kipindi cha saa 24.Inasemekana,maiti hizo zina alama zinazoonyesha kuwa wahanga hao waliteswa. Wakati huo huo maafisa wa kijeshi wa Kimarekani, siku nne kabla ya kufanywa uchaguzi wa baraza la Kongress la Marekani,wametangaza vifo vya wanajeshi wake wengine 5 nchini Irak.Vita vya Irak vimetawala kampeni za uchaguzi huo.Katika mwezi wa Oktoba,Marekani imepoteza wanajeshi 105 nchini Irak,hiyo ikiwa idadi kubwa kabisa tangu kuanza kwa vita hivyo.Hivi karibuni,wanajeshi 3 waliuawa katika mripuko wa bomu uliotokea kando ya barabara mjini Baghdad na mwengine aliuawa wakati wa mapigano katika wilaya ya Anbar.