1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Majeshi ya Iraq na Marekani yafanya msako wa nyumba kwa nyumba.

5 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCM8

Majeshi ya Iraq na yale ya Iraq leo yameingia katika eneo ambalo ni ngome ya wanamgambo wa Kishia mjini Baghdad , ambako mara ya kwanza walipambana katika mapigano makali ya mitaani , wakati mpango wao wa usalama unakabiliwa na mtihani mkubwa.

Operesheni hiyo inayohusisha mamia kadha ya wanajeshi katika kitongoji cha Sadr City , eneo ambalo hapo kabla lilikuwa haliingiliki likidhibitiwa na wanamgambo wa Kishia , inakuja wakati kuna mzozo kutokana na uvamizi dhidi ya wizara ya mambo ya ndani mjini Basra uliofanywa na majeshi ya Iraq na yale ya muungano hali ambayo ilimkasirisha waziri mkuu Nuri al-Maliki.

Msako huo ambao unafanywa nyumba kwa nyumba katika kitongoji hicho cha Sadr City ni mtihani kwa serikali ya al-Maliki ili kuweza kuunga mkono majeshi ya muungano ambayo yanajaribu kupambana na wanamgambo wa Kishia katika eneo ambalo ni ngome kuu ya mshirika wake , kiongozi wa kidini ambaye anaipinga Marekani Moqtada al-Sadr.