1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Majeshi ya Marekani kuondoka ifikapo 2007.

1 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCng

Waziri mkuu wa Iraq Nuri al-Maliki amesema kuwa majeshi ya nchi hiyo yatakuwa na uwezo kuchukua jukumu la ulinzi kutoka kwa majeshi ya Marekani ifikapo Juni 2007, hatua ambayo inaweza kuiruhusu Marekani kuanza kuondoa majeshi yake.

Katika mkutano uliofanyika nchini Jordan, rais wa Marekani George W. Bush amesisitiza kuwa majeshi ya Marekani yatabaki nchini Iraq kwa muda ambao serikali ya Iraq itayahitaji.

Mazungumzo yao yameingiliana na ghasia zaidi za kimadhehebu katika mji wa Baghdad.

Maafisa wa Iraq na wale wa Marekani wanasema kuwa miili ya karibu watu 80 wahanga wa mauaji imepatikana ilikiwa imeteswa na alama za kupigwa risasi.

Kiasi watu 15 pia wameuwawa mjini Baghdad jana Alhamis katika matukio kadha ya mashambulizi.