1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Majeshi ya Marekani yameua Washia

13 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjA

Majeshi ya Marekani yamevamia mtaa wanakoishi Washia wengi mjini Baghdad na kuwakamata wanamgambo wawili wanaoaminiwa kuwa na mahusiano na Iran.Kwa mujibu wa maafisa wa Kiiraqi,watu 19 waliuawa katika mapambano yaliyozuka.Miongoni mwa wale waliouawa ni waandishi wa habari 2 wa Kiiraqi.Lakini duru za kijeshi za Marekani hii leo zimesema,ni wanamgambo 9 na raia 2 waliouawa katika mapigano hayo.Tangu mwezi uliopita,katika juhudi ya kutaka kurejesha usalama,vikosi vya Marekani vinachukua hatua kali dhidi ya wanamgambo wa madhehebu ya Kishia na Kisunni, ndani na ukingoni mwa mji mkuu Baghdad.Hata hivyo lakini,polisi imeripoti kuwa siku ya Alkhamisi imegundua maiti 28 zingine katika sehemu mbali mbali za mji mkuu.Maiti hizo ni za watu waliotekwa nyara.