1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad: Mapigano makali mjini Baghdad, Iraq, baina ya majeshi ya serekali na waasi wa Kisunni

9 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CBHW

Mapigano makali ya bunduki yanafanyika sasa mjini Baghdad katika kile kinachoaminiwa kuwa ni msako mkali wa jeshi la Iraq dhidi ya waasi wa Kisunni. Wanajeshi wa Iraq wanasaidiwa na ndege pamoja na helikopta za jeshi la Marekani ambazo zinaonekana zikiruka juu ya anga ya mtaa wa Haifa ulio ngome ya watu wa madhehebu ya Sunni. Mapigano yalianza tangu alfajiri ya leo, na ilipofika mchana yalipamba moto. Polisi wanasema mapambano yalizuka pale watu walio na bunduki walipovishambulia vizuizi vya jeshi barabarani, na kwa hivyo wanajeshi wa Iraq waliomba msaada kutoka jeshi la Marekani.