1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mapigano makali yaendelea

11 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAo

Wanajeshi wa Marekani na Irak wamekabilaiana na wapiganaji katika mji mkuu Baghdad kwenye mapigano yanaoelezwa kuwa makali zaidi kuwahi kutokea tangu operehseni ya usalama ilipoanzishwa mnamo mwezi Februari mwaka huu.

Jeshi la Marekani limesema wanajeshi wanne wa Irak wameuwawa na wanajeshi 16 wa Marekani kujeruhiwa. Wapiganaji watatu wameuwawa kwenye mapigano hayo.

Helikopta mbili zilipigwa risasi na wapiganaji lakini zikafaulu kurejea kambini.

Wakati huo huo, mwanamke aliyejifunga mabomu alijiripua na kuwaua makurutu 17 nje ya kituo cha polisi mjini Mukdadiya yapata kilomita 90 kaskazini mashariki mwa mji mkuu Baghdad.

Sambamba na taarifa hizo, waziri mkuu wa Irak, Nuri al Maliki amekataa masharti ya bunge la Marekani kuweka tarehe ya wanajeshi wa Marekani kuondoka kutoka Irak.

Al Maliki akiwa ziarani nchini Japan, amesema serikali yake inafanya kila iwezalo kuimarisha usalama ili kuwawezesha wanajeshi wa Marekani na wanajeshi wengine wa kigeni waondoke kutoka nchini humo.