1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Marekani imeanzisha operesheni mpya ya kijeshi nchini Iraq

17 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqz

Vikosi vya Marekani nchini Iraq vimeanzisha operesheni mpya dhidi ya wanamgambo katika mji mkuu Baghdad.Kwa mujibu wa mkuu wa majeshi ya Marekani,Jemdari David Petraues,operesheni hiyo ya kijeshi inalenga ngome zinazotuhumiwa kuwa ni za Al-Qaeda.Waziri wa ulinzi wa Marekani,Robert Gates aliewasili Baghdad Ijumaa usiku kwa ziara ya ghafula,amekutana na Waziri Mkuu wa Iraq,Nuri al Maliki na pia wakuu wa majeshi ya Marekani.Waziri Gates alipoeleza kuhusu operesheni hiyo alisema kuwa ilianza siku chache zilizopita.Lakini utaratibu wa kuimarisha vikosi, ulianza tangu miezi kadhaa ya nyuma.Na „Kikosi cha 5“ kama sehemu ya operesheni hiyo,kilijiunga na mapigano hayo,siku chache zilizopita tu.