1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mashambulio nchini Irak yaendelea kupoteza maisha

19 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCrB

Nchini Irak,shambulio la kujitolea muhanga limeua hadi wafanyakazi 22 wa ujenzi katika mji wa Hilla ulio kama kilomita 120 kusini mwa mji mkuu Baghdad.Zaidi ya wafanyakazi wengine 40 walijeruhiwa pia.Mshambulizi aliekuwa ndani ya gari,alikaribia kundi la wafanyakazi,akijidai kuwa mkandarasi wa ujenzi alietaka kuwaajiri na akaliripua bomu alipozungukwa na wafanyakazi hao. Katika shambulio jingine lililotokea mashariki mwa mji wa Baquba,watu 8 waliuawa baada ya basi lililopakia wakulima kushambuliwa na waasi wa Kiiraki.