1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad: Mashambulio ya kujitoa mhanga yaendelea nchini Iraq.

2 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBco

Nchini Iraq, watu watano wameuawa baada ya shambulio la bomu la kujitoa mhanga kwenye kituo cha polisi katika mji wa Hibhib, kaskazini mwa Baghdad.

Maafisa wa usalama wamesema watu kumi na watatu wamejruhiwa kwenye shambulio hilo.

Shambulio hilo lilikuwa limelengwa watu waliokwenda kupeleka maombi ya kazi ya polisi.

Shambulio hilo limetekelezwa siku moja baada ya mashambulio kadhaa yaliyotukia mjini Baghdad na kusababisha vifo vya watu zaidi ya sabini.