1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mashambulizi ya bomu Irak yameua watu 6

18 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhZ

Watu 6 wameuawa na wengine 5 wamejeruhiwa katika miripuko miwili ya bomu iliyotokea kando ya barabara,kusini-mashariki ya mji mkuu wa Irak,Baghdad.Kwa mujibu wa polisi,mashambulizi hayo yamefanywa karibu na kituo cha petroli yanaposismama mabasi yanayotokea eneo la kusini wanakoishi Washia wengi.Majeshi ya Marekani na Irak yameimarisha operesheni za usalama ndani na ukingoni mwa Baghdad kwa azma ya kuzuia mapambano ya kikabila kati ya makundi ya Washia na Wasunni, hata hivyo lakini machafuko yanaendelea.