1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mashambulizi yameua raia 15 nchini Iraq

3 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvA

Wairaqi 15 wameuawa katika mashambulizi mawili mbali mbali,kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad.Shambulio la kwanza la bomu lililotegwa ndani ya gari,lililenga polisi waliokuwa wakipiga doria,lakini bomu hilo liliripukia soko la mboga na matunda.Raia 10 waliuawa katika shambulizi hilo.Na kwenye barabara kuu kati ya Muqdadiyah na Baghdad,raia 5 waliuawa na 7 walijeruhiwa baada ya watu wenye bunduki kusimamisha basi dogo na kuwafyatulia risasi abiria waliokuwemo ndani.