1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mashtaka dhidi ya Saddam yafutiliwa mbali

8 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcF

Mahakama kuu nchini Irak imefutilia mbali mashataka yote dhidi ya rais wa zamani Saddam Hussein, huku kesi ya mauaji ya Wakurdi ikianza kusikilizw aleo mjini Baghdad.

Saddam Hussein alinyongwa mnamo tarehe 30 mwezi Disemba 30 jana kwa mauaji ya Washia 148 katika kijiji cha Dujail mwaka wa 1982. Saddam Hussein na washukiwa wengine sita wameshtakiwa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu uliofanywa dhidi ya Wakurdi wa Irak wakati wa kampeni ya miaka ya 1980. Wakurdi zaidi ya 180,000 waliuwawa.

Mtuhumiwa mkuu katika kesi hiyo ni binamu yake Saddam, Ali Hassan al Majid, anayejulikana kwa jina maarufu la Chemical Ali.

Wakati huo huo, wafanyakazi wasiopungua 15 wameuwawa leo na wengine 15 weakajeruhiwa wakati lori walimokuwa wakisafiria kuelekea uwanja wa ndege wa Baghdad liliposhambuliwa.