1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Mauaji yaendelea Iraq

29 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCoQ

Nchini Iraq bomu limeripuka karibu na kituo cha basi cha jiji la Baghdad na kuuwa raia wawili.

Maafisa wa usalama wamesema bomu hilo limeripuka mapema leo hii na imeonekana kuwa lilikuwa limewalenga kundi la polisi lililokuwa likipita hapo.Polisi wawili walijeruhiwa kwenye mripuko huo pamona na watu wengine watano.

Kaskazini mwa mji mkuu huo genge la watu 40 wenye silaha lilikishambulia kituo cha ukaguzi cha polisi na kuuwa askari wawili na kujeruhi wengine wawili.