1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Moqtada al Sadr akimbilia Iran

14 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSN

Habari ambazo bado hazijathibitishwa zinasema shehe wa kishia mwenye siasa kali, Moqtada al Sadr, amekimbia Irak na sasa yuko Iran.

Kuondoka kwa al Sadr kumehusishwa na mpango wa rais Bush wa kuongeza wanajeshi 21,500 nchini Irak. Marekani imelitaja jeshi la Mehdi la Moqtada al Sadr, kama tisho kubwa kwa usalama wa Irak na imemtaka waziri mkuu wa Irak, Nuri al Maliki, alipokonye silaha.

Ripoti ya kukimbia kwa al Sadr imetolewa siku chache baada ya maofisa wa jeshi la Marekani mjini Baghdad kuwaonyesha waandishi wa habari makasha ya silaha walizosema zimetengenezwa nchini Iran na kusema maofisa ngazi ya juu katika serikali ya Iran wanahusika katika kuwapa silaha wapiganaji wa Irak.