1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Msako wa usalama wapamba moto

9 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTm

Katika ishara ya kwanza kwamba msako mkubwa wa usalama unafanyika mjini Baghdad wanajeshi wa Marekani na wale wa Iraq wamemtia mbaroni naibu waziri wa afya wa Iraq ambaye ni mfuasi wa Sheikh wa Kishia Moqtada al Sadr.

Marekani inamtuhumu waziri huyo kwa vitendo vya utekaji nyara na kuwapatia wanamgambo mamilioni ya dola.Wakati huo huo katika umwagaji damu wa kimadhehebu wa hivi karibuni kabisa watu wenye silaha wamewapiga risasi na kuwauwa watu 14 kutoka familia moja ya Kisunni kaskazini mwa Baghdad.Bomu lililotegwa kwenye gari limeuwa watu 17 kwenye soko katika mji wenye Washia wengi kusini mwa Baghdad na wanajeshi wa Marekani wamewauwa waasi 13 katika shambulio la anga magharibi mwa mji mkuu huo.

Hapo jana takriban watu 20 wameuwawa na mapema kutokana na mripuko wa bomu lililotegwa kwenye gari katika mji wa Al- Aziziya ulioko kilomita 70 kusini mashariki mwa Baghdad.