1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Msikiti wa Samarra waliripuliwa tena

14 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBrx

Viongozi wa Kishia wametowa wito wa kuwepo kwa utulivu baada ya wanamgambo wanaotuhumiwa kuwa wa kundi la Al Qaeda kuripuwa minara miwili ya msikitiki mtakatifu wa Kishia katika mji wa Samarra.

Mripuko huo umetokea licha ya kuwepo kwa ulinzi wa kudumu kwenye msikiti huo wa Al Askari.Mripuko kwenye msikiti huo huo ambao pia unajulikana kama msikiti wa dhahabu miezi 15 iliopita ulichochea mauaji ya kimadhehebu nchini kote Iraq.

Muda mfupi baada ya mripuko huo wa jana msikiti minne ya Wasunni ilishambuliwa kutokana na kile kinachonekana kuwa ni kulipiza kisasi.

Serikali ya Iraq imetangaza amri ya kutotembea nje katika mji wa Samarra na Baghad katika jaribio la kuzuwiya umwagaji damu zaidi.