1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mwito kwa kukomesha mmuagiko wa damu

6 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5j

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice ametoa wito kwa viongozi wa makundi mbali mbali ya kisiasa nchini Irak kuweka kando tofauti za maoni yao.Alipozungumza na viongozi wa serikali ya waziri mkuu Noori al-Maliki mjini Baghdad,Rice amesema viongozi hao wanapaswa kukomesha mapambano ya kila siku kati ya makundi ya kidini nchini humo.Uhaba wa usalama na vifo mia moja vinavyotokea kila siku kwa sababu ya mashambulio ni hali isiyoweza kustahmiliwa.