1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Naibu waziri mkuu ajeruhiwa

24 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCG3

Naibu waziri mkuu wa Iraq Salam al-Zubayi yuko mahtuti baada ya kujeruhiwa katika shambulio la kujitowa muhanga maisha kwa kujiripuwa katika msikiti wa Baghdad ulio karibu na nyumba yake.

Polisi inasema takriban watu tisa wameuwawa katika shambulio hilo na wengine zaidi ya 12 kujeruhiwa.Mshambuliaji huyo alijiripua wakati Zubayi na waumini wengine walipokuwa wakiondoka msikitini katika eneo lenye ulinzi mkali la Ukanda wa Kijani ambayo ni makao makuu ya serikali.Polisi imesema gari lilioegeshwa karibu liliripuka wakati huo huo.

Kuna tetesi kwamba shambulio hilo dhidi ya naibu waziri mkuu huyo wa madhehebu ya Sunni yumkini likawa limetokana na habari zilizotoka ndani ya ofisi yake.