1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Polisi wapambana na majeshi ya Moqtada al-Sadr.

23 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgj

Watu sita wameuwawa na wengine 15 wamejeruhiwa katika mapigano kati ya polisi wa Iraq na wapiganaji wanaomuunga mkono kiongozi mhafidhina wa Kishia Moqtada al-Sadr.

Mapigano hayo yalizuka wakati maafisa wa Iraq walipokataa wanamgambo wasichukue silaha wakati wa sala ya Ijumaa, na mapigano hayo yaliendelea baada ya polisi kuwakamata watu kadha.

Marekani imemlaumu Sadr na wanamgambo wake kwa kuchochea ghasia za kimadhehebu ambazo zinatokea nchini Iraq hivi sasa.