1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Polisi wauwawa na majeshi ya Marekani.

14 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBiv

Wanajeshi wa Marekani wamewauwa polisi sita wa Iraq baada ya kushambuliwa kwa risasi kutoka katika kituo cha polisi cha upekuzi mjini Baghdad, jeshi la Marekani limesema.

Watu saba wanashukiwa kuwa ni wapiganaji pia wameuwawa katika mapambano hayo.

Wanajeshi wa Marekani wamemkamata luteni mmoja wa polisi kwa tuhuma za kupanga shambulio la bomu la kando ya barabara na shambulio la kombora dhidi ya majeshi ya Marekani.

Rais George W. Bush wa Marekani ameelezea juhudi za ujenzi mpya nchini Iraq jana ,wakati akipambana kuvuta muda kwa ajili ya mkakati wake unapoteza uungwaji mkono baada ya kutolewa ripoti isiyoonyesha matumaini pamoja na kushambuliwa vikali na baraza la Congress.

Siku moja baada ya baraza la wawakilishi kupiga kura kuondoa idadi kubwa ya majeshi ya Marekani kuazia mwezi wa Aprili mwakani , rais Bush alizungumza na makamanda mjini Baghdad na Washington kuelezea msimamo wake kuwa Marekani inaweza kushinda vita na lazima ishinde.

Wakati huo huo , ripota mmoja wa Iraq anayefanyakazi na gazeti la The New York Times alipigwa risasi na kufa wakati akiwa njiani kwenda kazini mjini Baghdad, gazeti la Times limesema, siku moja baada ya wafanyakazi wawili wa shirika la habari la Reuters kuuwawa wakati wa tukio lililohusisha majeshi ya Marekani mjini humo.