1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad . Rumsfeld atembelea majeshi Iraq.

10 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCki

Waziri wa ulinzi wa zamani wa Marekani Donald Rumsfeld amekwenda Iraq katika ziara ya ghfla ili kuwashukuru wanajeshi wa Marekani kwa kazi yao.

Taarifa za ziara ya Rumsfeld zinakuja siku tisa kabla ya wadhifa wake kuchukuliwa na Robert Gates, kiongozi wa zamani wa shirika la ujasusi la Marekani CIA.

Rumsfeld amejiuzulu mwezi Novemba , siku baada ambacho chama cha rais George W. Bush cha republican kilishindwa kudhibiti baraza la Congress wakati wapigakura wakikerwa na suala la vita vya Iraq likitawala uchaguzi huo.