1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Serikali ya Irak itapangwa upya majuma yajayo

4 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMN

Waziri mkuu Nouri al-Maliki wa Irak amesema,ataipanga upya serikali yake katika kipindi cha majuma mawili yajayo,lakini hakutoa maelezo zaidi.Inatazamiwa kuwa vyeo vya mawaziri ambavyo hivi sasa ni 39,vitapunguzwa.Akaongezea kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wanasiasa wenye uhusiano na wanamgambo.Ingawa majuma matatu ya nyuma vikosi vya Irak na Marekani vilianzisha operesheni maalum kujaribu kurejesha usalama mjini Baghdad,hali ya usalama haikubalika sana katika mji huo mkuu.