1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Shambulio dhidi ya polisi lauwa 9

22 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7z

Watu 9 wameuwawa na 28 kujeruhiwa mjini Baghdad na washambuliaji wawili wa kujitolea muhanga maisha walioyabamiza magari yao dhidi ya kituo cha polisi.

Watu 10 waliojeruhiwa ni maafisa wa polisi.Shambulio hilo limetokea katika kiunga cha Bayaa kinachokaliwa zaidi na Washia.

Waasi wamekuwa wakizidi kutumia mashambulizi ya mabomu katika mji mkuu huo wa Iraq licha ya kuwepo kwa msako mkubwa wa usalama unaohusisha maelfu ya wanajeshi wa Marekani na Iraq.