1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Shambulio la jeshi la Marekani laua watu wa familia moja.

8 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClM

Kiasi cha watu 20 wa familia moja kubwa wanaaminika kuwa wameuwawa katika mashambulizi ya anga ya jeshi la Marekani kaskazini mwa Iraq leo Ijumaa.

Shambulio hilo lilifanyika katika eneo la Is- haki karibu na ziwa Tharthar, kiasi cha kilometa 70 kutoka mji wa Tikrit.

Meyaa wa mji wa Is- Haki Amer Aluan amesema kuwa watu wanne walifyatua risasi dhidi ya jeshi la Marekani mchana kabla ya kupigwa risasi na jeshi hilo na kufa na nyumba zao kuvamiwa. Meya huyo amesema wakati majeshi hayo ya Marekani yakishambulia nyumba mbili za ndugu Mahmoud Hussein Galmoud na Mohammed Hussein Galmoud, pia waliwapiga risasi na kuwauwa watoto kumi wenye umri wa kuazia miaka miwili hadi 14 pamoja na wanawake wanne. Watu watatu hawajulikani waliko.