1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Shambulizi la kujitolea muhanga lasababisha hadi vifo 30

7 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBl8

Watu wasiopungua 30 wameuawa katika mripuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari,katika eneo la sokoni mjini Tuz Khurmato,kaskazini mwa Iraq.Kwa mujibu wa polisi,watu 80 vile vile walijeruhiwa katika shambulizi hilo la kujitolea muhanga kwenye soko la hadhara lililojaa watu.Mripuko huo pia umeteketeza idadi kadhaa ya majengo yaliokuwepo karibu na eneo hilo.Inahofiwa kuwa huenda ikawa watu wamegubikwa na vifusi vya majengo yaliyoporomoka.