1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Takriban watu 30 wameuwawa

9 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBav

Takriban watu 30 wameuwawa katika shambulio la ndege za kijeshi za Marekani dhidi ya mji wa Sadr.

Jeshi la Marekani limetoa taarifa kwamba shambulio hilo liliwalenga wanamgambo wenye msimamo mkali ambao wanahusika na uingizaji silaha kinyume cha sheria kutoka nchini Iran.

Polisi na watu walioshuhudia shambulio hilo wamesema kwamba raia tisa waliuwawa katika shambulio hilo.

Wakati huo huo wazairi mkuu wa Irak Nuri al malik amepokea hakikisho kutoka nchi jirani ya Iran kwamba inafanya jitihada za kuleta utulivu nchini Irak.

Makamu wa rais wa kwanza wa Iran Parviz Davoudi ameaysema hayo wakati wa mkutano kati yake na bwana Maliki ambae ameanza ziara ya siku tatu mjini Tehran.

Waziri mkuu wa Irak Nuri al Maliki anafanya ziara hiyo nchini Iran siku mbili baada mkutano wa kamati ya maafisa wa Iran, Irak na Marekani kukutana mjini Baghdad na kujadili juhudi za pamoja zenye lengo la kuleta utulivu nchini Irak.