1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Umwagaji damu unaendelea nchini Irak

25 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOe

Roketi mbili zimeangukia kusini mwa mji mkuu wa Irak Baghdad ambako Washia wengi huishi.Si chini ya watu 12 wameuawa na 8 wengine wamejeruhiwa. Hapo kabla,mripuko uliotokea katika eneo lenye ulinzi mkali katikati ya Baghdad,uliua watu wasiopungua 2 na kuwajeruhi watu 8.Machafuko hayo yanatokea huku waziri mkuu wa Irak,Nouri al-Maliki akidai kuwa maendeleo yanapatikana kupiga vita uasi mjini Baghdad na kwamba hali ya usalama imekuwa bora.Ripoti zingine zinasema kuwa vikosi vya anga vya Marekani vimeshambulia vituo vinavyosemekana kuwa ni vya waasi.Kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Irak,Nouri al-Maliki,zaidi ya waasi 400 wameuawa tangu kuanzishwa kwa operesheni ya kuleta usalama mjini Baghdad.