1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Umwagaji damu waendelea nchini Iraq

1 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBwA

Nchini Iraq hadi watu 20 wameuawa na wengine dazeni kadhaa wamejeruhiwa katika shambulizi la kujitolea muhanga,kwenye kituo cha kusajili askari polisi wapya,mjini Fallujah.Kwa mujibu wa polisi,mtu mmoja alijiripua kwa bomu alipokuwa akisimama foleni na raia wengine waliotaka kuajiriwa kazi ya polisi.Kwa upande mwingine, waziri wa ulinzi wa Marekani,Robert Gates amesema,Marekani inafikiria mpango wa kuvibakisha vikosi vyake nchini Iraq kwa muda mrefu kwa makubaliano ya pande mbili sawa na yale yaliopo pamoja na Korea ya Kusini.Vikosi vya Marekani vipo Korea ya Kusini tangu kumalizika kwa vita vya Korea hapo mwaka 1953.