1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Umwagaji damu waendelea nchini Iraq

8 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3z

Hadi watu 20 wameuawa nchini Iraq katika mashambulio mawili ya kujitolea muhanga na kuripua mabomu yaliyotegwa ndani ya gari.Zaidi ya watu 40 pia walijeruhiwa katika mashambulio hayo katika mji wa Ramadi.Bomu la kwanza liliripuka katika soko linalotumiwa na watu wengi,kaskazini ya Ramadi.Dakika 15 baadae,bomu la pili liliripuliwa karibu na mlolongo wa watu waliosimama mbele ya kituo cha ukaguzi cha polisi.Watu wengine 10 waliuawa katika shambulio hilo la pili.