1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad: Umwagaji damu zaidi Iraq

7 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLW

Mashambulio dhidi ya Washia nchini Irak yameendelea leo, wakati miripuko ya mabomu na mapigano ya risasi yaliposababisha watu 11 kuwawawa kusini mwa mji mkuu Baghdad. Bomu lililotegwa barabarani liliripuka kandoni mwa mahujaji waliokua wakisafiri kwenda Karbala, kabla ya sikukuu ya washia mwishoni mwa juma, kukumbuka kifo cha Imam Hussein, mjukuu wa Mtume Muhammad. Imam Hussein alifariki karibu na Karbala wakati wa mapigano mnamo karne ya saba. Kwa mujibu wa polisi, kiasi ya watu 7 waliuwawa na wengine 14 kujeruhiwa katika shambulio la bomu katika eneo la Dora linalokaliwa kwa sehemu kubwa na wawasunni kusini mwa Baghdad.

Saa chache baadae watu waliokua na silaha wakawafyatulia risasi mahujaji wa Kishia kwenye daraja moja kusini mashariki mwa mji huo mkuu, wakiwauwa watu 3 na kuwajeruhi wengine watano. Mtu mmoja mwengine akauwawa katika mapigano ya risasi kati kati ya Baghdad.Hujuma za leo zinafuatia mbili za kujitoa mhanga jana ambapo karibu watu 120 waliuwawa. Watu hao walikua miongoni mwa umati mkubwa wa mahujaji wa washia .