1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Utulivu kupatikana Iraq

25 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzT

Balozi wa Marekani nchini Iraq amewahakikishia wapiga kura wa Marekani kwamba utulivu unaweza kupatikana katika nchi hiyo iliokumbwa na vita.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Baghdad akiwa pamoja na Kamanda mkuu wa majeshi ya Marekani nchini Iraq Generali George Casey Balozi Zalmay Khalilzad ameyeelezea mapambano yanayoendelea dhidi ya umwagaji damu wa kimadhehebu na uasi nchini Iraq kuwa ni kielelezo cha changamoto katika enzi yao.Khalilzad amezishutumu Iran na Syria kwa kuunga mkono kundi la kigaidi la Al Qaeda katika majaribio ya kuivuruga Iraq na kuzuwiya Marekani kuanzisha demokarasia imara nchini humo.

Generali Casey amewaambia waandishi wa habari kwamba vikosi vya Iraq vinazidi kuchukuwa majukumu ya usalama na kwamba kukabidhiwa madaraka kamili kwa vikosi hivyo kunaweza kufanyika katika kipindi cha miezi 12 hadi 18.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Tony Snow amesema serikali ya Marekani katu haikuwahi kuiwekea tarehe ya mwisho Iraq kutekeleza mambo na kutishia kuondowa vikosi vyake nchini humo.