1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Vikosi vya Irak kulinda usalama Kerbala

29 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7BW

Vikosi vya usalama vya Irak,vimepokea rasmi dhamana ya ulinzi katika wilaya ya Kerbala ambako kuna miji mitakatifu kwa Waislamu wa madhehebu ya Kishia.Vile vile makundi ya Kishia yamekuwa yakipigana katika kinyanganyiro cha madaraka ya kisiasa katika eneo hilo.

Sasa vikosi vya Kiiraki vimeshapewa na Marekani dhamana ya kulinda usalama katika wilaya 8 kutoka jumla ya wilaya 18 nchini Irak.