1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Wafanyakazi wa shirika la hilali nyekundu waachiliwa huru

19 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChz

Watekaji nyara wamewaachilia huru wafanyakazi 26 kati ya wafanyakazi 30 wa shirika la hilali nyekundu mjini Baghdad. Wafanyakazi hao walitekwa nyara siku mbili zilizopita mjini Baghdad.

Msemaji wa shirika la hilali nyekundu amesema anatarajia kwamba wafanyakazi wengine waliosalia wataachiliwa huru wakati wowote.

Watu waliokuwa na bunduki walizivamia ofisi za shirika la hilali nyekundu mjini Baghdad mnamo Jumapili iliyopita na kuwateka nyara wafanyakazi wa kiumue wakidai walikuwa wakifanya uchunguzi.