1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD :Wafanyikazi wa ulinzi waua watu 9

17 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPB

Wafanyikazi wa kampuni moja ya ulinzi wamewapiga risasi yapata wakazi 9 hadi kufa na wengine 18 kujeruhiwa mjini Baghdad.Kulingana na ubalozi wa marekani nchini humo wafanyikazi wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani walihusika katika tukio hilo ila hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.Mauaji hayo yalifanyika katika eneo la Mansour mtaa wa Nisoor ulio na Wasunni wengi kulingana na afisa mmoja wa polisi ambaye hakutaka kutambuliwa.Wafanyikazi hao wa usalama walikuwa katika msafara wa magari sita na kuondoka mahala hapo pa mkasa baada ya tukio lenyewe.

Wanajeshi wa Marekani walifika katika eneo hilo la mkasa lakini hawakuhusika kwa mujibu wa msemaji wa jeshi Luteni kanali Scott Bleichwehl.Waziri mkuu wa Iraq Nuri al Maliki alishtumu kitendo hicho.