1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Wanajeshi 9 wa Marekani wauwawa

24 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7g

Wanajeshi tisa wa Marekani wameuwawa na 20 kujeruhiwa katika shambulio la kujitolea muhanga maisha kwa kujiripuwa kwenye gari dhidi ya kituo cha doria kaskazini mashariki ya Baghdad leo hii.

Shambulio hilo limetokea katika jimbo la Diyala eneo tete ambalo limekumbwa na mapigano kati ya wanajeshi wa Marekani wakishirikiana na vikosi vya Iraq dhidi ya waasi wa Kusunni na wanamgambo wa Kishia.

Takriban watu 19 wameuwawa hapo jana katika shambulio la bomu lililotegwa kwenye gari karibu na mkahawa katika mji wa magharibi wa Ramadi.Kwa mujibu wa polisi zaidi ya watu 30 walijeruhiwa katika mripuko huo.

Wanajeshi wa Marekani walipokimbilia kwenye eneo hilo waligunduwa gari lililoegeshwa karibu na hapo likiwa limesheheni mabomu na gesi ya klorin ambalo baadae waliliteketeza kwa kuliripua.