1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Wanajeshi tisa wa Marekani wauwawa Irak

18 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1h

Jeshi la Marekani limesema wanajeshi wake tisa wameuwawa leo katika mapigano mbalimbali mjini Baghdad, Irak wanajeshi wanne wameuwawa wakati gari lao lilipolipuliwa na bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara magharibi mwa Baghdad.

Wanajeshi wengine watatu wameuwawa wakati wa mapigano yaliyozuka katika wilaya ya Diyala mashariki mwa mji huo.

Mwanajeshi mwingine ameuwawa katika uvamizi uliofanywa na wapiganaji wa Irak dhidi ya kikosi chao kaskazini mwa Baghdad na mwengine akafariki kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa mapigano katika mkoa wa Al Anbar.

Idadi ya wanajeshi wa Marekani waliouwawa mwezi huu imefikia 67.