1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Wanajeshi wa Marekani wawatafuta wanajeshi wenzao.

13 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2Y

Majeshi ya Marekani yameanzisha msako mkubwa kuwatafuta askarijeshi wao watatu wanaohofiwa huenda walitekwa nyara na wanamgambo baada ya shambulio lililosababisha vifo vya askarijeshi wengine watano.

Majeshi ya Marekani yamesema wanajeshi saba waliokuwa wakishika doria pamoja na mtapta wao raia wa Iraq walishambuliwa karibu na mji wa Mahmudiyah kiasi kilomita thelathini kusini mwa mji mkuu, Baghdad.

Taarifa zinasema majeshi ya Marekani yamevamia maeneo ya mashambani kusini mwa Baghdad kuwatafuta wanajeshi wenzao waliotekwa.

Meya wa Mahmudiyah, Moad al-Amiri amesema majeshi hayo yamelizingira eneo hilo na yamewatia nguvuni washukiwa kiasi hamsini.

Kwa mujibu wa meya huyo, wanajeshi wa Iraq hawajahusishwa kwenye msako huo wa Wamarekani.

Mji wa Mahmudiya ndio ngome kuu ya wanamgambo wa Kisunni.