1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Wanajeshi wa ziada wa Marekani waanza kuwasili Irak

15 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaK

Wanajeshi wa ziada wa Marekani wameanza kuwasili nchini Irak. Kamanda wa jeshi la Marekani nchini humo, jenerali George Casey, amethibitisha hayo mjini Baghdad wakati wa mkutano na waandishi wa habari akiwa ameandamana na balozi wa Marekani nchini Irak, Zalmay Khalilzad.

Jenerali Casey amesema bado kuna tatizo na vikosi vya Irak. ´Hapa bado kuna matatizo na vikosi vya usalama vya Irak na hilo limekuwa changamoto. Kuongezwa kwa idadi ya wanajeshi kutazipiga jeki juhudi za kuvisaidia vikosi hivyo, kuvipa nguvu kidogo kadri tunavyoendelea kuutekeleza mpango mpya wa Irak.´

Jenerali Casey ameongeza kusema kwamba mpango mpya wa Marekani kuviimarisha vikosi vyake nchini Irak hauna uhakika wa kufaulu na ufanisi hautapatikana kwa haraka. Hata hivyo anaamini mpango huo utapiga hatua kama juhudi zaidi za kisiasa zitafanywa.

Aidha jenerali Casey amesema mpango huio ni fursa kwa Wairaki kujitokeza na kuvisaidia vikosi vyao vya usalama ili kuiendeleza nchi yao.