1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Wanajeshi watatu wa Marekani wauawa nchini Iraq.

20 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZP

Majeshi ya Marekani nchini Iraq yamearifu askari wake watatu wameuawa kwenye mashambulio tofauti nchini humo.

Askari mmoja aliuawa kwenye mripuko wa bomu lililotegwa kando ya barabara kaskazini mwa Baghdad, ilhali askari mwengine aliuawa katika jimbo la Anbar.

Wakati huo huo taarifa zinasema wanamgambo wamewaua watu sita katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo, akiwemo kanali wa Jeshi la Iraq.