1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Wanajeshi watatu zaidi wa Marekani wauwawa.

5 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCK

Jeshi la Marekani nchini Iraq limeripoti kuwa wanajeshi wake watatu zaidi wameuwawa mjini Baghdad. Wawili miongoni mwa wanajeshi hao waliuwawa wakati bomu lililotegwa kando ya barabara lilipolipuka karibu na magari ya doria.

Mwanajeshi wa tatu alipigwa risasi na wapiganaji.

Kwingineko nchini Iraq, kwa mujibu wa jeshi la Uingereza mabomu mawili yaliyotegwa kandoni mwa barabara yaliwalipukia wanajeshi wa jeshi la Uingereza katika ngome ya wanamgambo wa Kishia kusini mwa Iraq katika mji wa Basra na kuuwa wanajeshi wanne pamoja na mkalimani wao raia wa Iraq.