1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Wanakijiji 11 wa Kishia wauwawa

25 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpL

Watu wenye silaha wamewaua wanakijiji 21 wa madhehebu ya Shia wakati umwagaji damu wa kimadhehebu ukiendelea nchini humo.

Watu hao wanaotuhumiwa kuwa waasi walizivamia nyumba mbili katika jimbo la Diyala kaskazini mashariki mwa Baghdad na kuwaburuza nje wanaume 21 na baadae kuwapiga risasi. Mashambulizi hayo yamekuja kufuatia wiki ya umwagaji damu mkubwa mjini Baghdad ambapo kwayo zaidi ya watu 200 wameuwawa kutokana na miripuko ya mabomu na mapigano katika wilaya ya mji wa Sadr.

Mji mkuu wa Baghdad umeendelea kuwa chini ya amri ya kutotembea nje kwa siku ya pili.

Rais Jalal Talabani wa Iraq amelazimika kuahirisha ziara yake kwa Iran kwa sababu ya uwanja wa ndege wa Baghdad pia umefungwa.

Amesema atafanya safari katika nchi hiyo jirani ya Iran kwa mazungumzo juu ya dhima inayowezekana kutimizwa na nchi hiyo katika kusaidia kuzuwiya umwagaji damu nchini Iraq mara tu uwanja wa ndege huo utakapofunguliwa.