1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Wapiganaji 17 wauwawa.

29 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCy2

Majeshi ya Marekani na yale ya Iraq yamesema kuwa yamewauwa wapiganaji 17 katika mapigano kaskazini mwa Baghdad.

Jeshi hilo limesema mlolongo wa jeshi la Marekani na Iraq ulishambuliwa na kundi la watu wenye silaha.

Wakati huo huo watu wenye silaha walifyatua risasi dhidi ya msafara wa magari ya serikali katika mji mkuu wa Baghdad na kumjeruhi mlinzi mmoja wa waziri mkuu Nouri al-Maliki, ambaye hakuwa katika msafara huo wakati ukishambuliwa.