1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Wapiganaji 30 wauwawa na majeshi ya serikali.

7 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCce

Jeshi la Iraq limeripoti kuwa limewauwa wapiganaji 30 katika mapigano katikati ya mji wa Baghdad. Televisheni ya taifa ya Iraq imesema kuwa wapiganaji wanane , ikiwa ni pamoja na wapiganaji watano raia wa Sudan , wamekamatwa katika mapigano hayo karibu na mtaa wa Haifa, eneo ambalo ni ngome ya Wasunni.

Polisi wameripoti kuwa wamegundua miili ya watu 71 ambayo wameteswa kabla ya kuuwawa na kuachwa katika eneo mapema jana.

Uwekaji wa jeshi katikati ya mji huo mkuu unaaminika kuwa ni mwanzo wa msukumo mpya wa usalama mjini Baghdad, uliotangazwa saa chache zilizopita na waziri mkuu Nouri al-Maliki.

Msaidizi maalum wa waziri huyo mkuu amesema kuwa kiongozi huyo ameamuru wanajeshi 20,000 kufanya operesheni hiyo ambayo itapata msaada wa jeshi la Marekani ikiwa litahitajika.