1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD :Washambulizi wamemuua mkuu wa idara ya chuo kikuu

2 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwe

Mkuu wa kitivo katika chuo kikuu cha Baghdad ameuawa kaskazini mwa mji mkuu wa Irak Baghdad baada ya kupigwa risasi na watu waliopita kwa gari.Jasim al-Thahabi alikuwa mkuu wa idara ya uchumi katika chuo kikuu cha Baghdad.Mkewe na mtoto wake wa kiume pia wameuawa katika shambulio hilo.Siku tatu za nyuma pia washambulizi walimuua mkuu wa kidini wa madhehebu ya Kisunni,Issam al-Rawi aliekuwa na siasa za wastani.Al-Rawi alikuwa mkuu wa jumuiya ya walimu wa chuo hicho kikuu.