1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Watu 150 watekwa nyara

14 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsm

Watu wenye silaha wakiwa wamevalia sare za polisi wa Iraq wamewateka nyara takriban watu 150 katika utekaji nyara wa kundi kubwa kabisa la watu kuwahi kushuhudiwa kwenye mkuu wa nchi hiyo Baghdad tokea Marekani ilipoivamia nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shahidi wa tukio hilo polisi walikuwa wamekaa pembeni wakiangalia wakati wateka nyara hao wakikaguwa vitambulisho kwa kuwatofautisha Wasunni na Washia na baadae kuondoka na wanaume wa Kisunni kutoka taasisi ya utafiti mjini Baghdad.

Kufuatia tukio hilo waziri wa elimu ya juu nchini Iraq Abed Dhiab ameamuru kufungwa kwa vyuo vyote vikuu nchini humo hadi hapo hali ya usalama itakapokuwa nzuri.Waziri huyo amesema hayuko tayari kuona maprofesa zaidi wakiuwawa.

Amesema amekuwa mara kwa mara akizitaka wizara za mambo ya ndani na ulinzi kuweka ulinzi katika vyuo vikuu lakini ombi lake lake limeshindwa kutekelezwa.

Oporesheni hiyo ya utekaji nyara imedumu kwa dakika 10 hadi 15 na wateka nyara hao walikuwa na takriban magari 20.