1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Watu 36 wauwawa nchini Iraq

6 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbe

Nchini Iraq takriban watu 36 wameuwawa katika shambulio la kujitolea muhanga maisha kwenye mji wa magharibi wa Tal Afar na mjini Baghdad.

Shambulio hilo katika kitongoji cha Washia limetokea wakati lori lilosheheni mabomu liliporipuliwa katika eneo lilojaa watu. Msemaji wa jeshi amesema takriban watu 28 wameuwawa na wengine 50 kujeruhiwa katika shambulio hilo.Idadi ya vifo inategemewa kuongezeka.

Mripuko wa bomu mjini Baghdad umeuwa watu tisa.

Serikali ya Iraq imeweka amri ya kutotembea nje katika mji huo. Wakati huo huo serikali ya Marekani imesema mkakati wake wa kijeshi wa kutuma wanajeshi 30,000 wa ziada nchini Iraq umekuwa na mafanikio lakini imelalamika juu ya kushindwa kwa wanasiasa wa Iraq kupiga hatua za maendeleo katika kufanikisha usuluhishi wa kitaifa kati ya Waislamu walio wengi wa madhehebu ya Shia na wale walio wachache wa madhehebu ya Sunni.