1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Watu 40 wauwawa kwa mlipuko wa bomu.

12 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJu

Mabomu mawili ya kujitoa muhanga katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad , umesababisha kiasi watu 40 kuuwawa.

Katika tukio baya kabisa , mtu aliyekitoa muhanga katika gari aliigonga gari yake katika lori lililokuwa likiwarejesha mahujaji wa Kishia kutoka katika mji wao mtakatifu wa Kerbala, na kuuwa kiasi watu 30.

Mlipuko mwingine ulilenga dhidi ya basi dogo mashariki ya Baghdad.

Mashambulio ya jana Jumapili yanafuatia wiki moja ambapo mamia ya mahujaji wa Kishia waliuwawa wakijaribu kwenda Kerbala kwa ajili ya sherehe muhimu za kidini.

Wakati huo huo , jeshi la Marekani limesema kuwa wanajeshi watano wa jeshi lake wameuwawa nchini Iraq, watatu ikiwa ni katika mapambano na wawili katika matukio ambayo si mapigano ya moja kwa moja.